Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

De Ligt kufungwa jela

De Lights De Ligt kufungwa jela

Sun, 11 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Bayern Munich ambaye anawindwa na Manchester United, Matthijs de Ligt anadaiwa kuwa chini ya uchunguzi wa polisi wa Ujerumani kwa tuhuma za kugonga na kukimbia.

Staa huyu ambaye aliachwa nje ya kikosi cha Bayern Munich kilichosafiri kwenda Korea Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu, yupo katika rada za Man United ambayo imezidisha nguvu baada ya kuumia kwa Leny Yoro.

Ripoti kutoka tovuti ya BILD, zinaeleza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anadaiwa kuwa aligonga gari lililoegeshwa karibu na uwanja wa mazoezi wa  Bayern, Sabener Strasse, Jumatano asubuhi alipokuwa akiendesha gari lake aina ya Audi Q8 yenye thamani ya Pauni 63,000.

Chombo cha habari cha Ujerumani kinadai kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi mara baada ya kugonga aliondoka bila ya kusubiri chochote.

Baadhi ya mashahidi waliokuwepo eneo hilo walipiga simu polisi na haikuchukua muda De Ligt alikamatwa na gari yake ikachukuliwa.

Kwa mujibu wa wakili kutoka jiji la Munich, Marc Wederhake, De Ligt anaweza kukabiliwa na kifungo kama ama akatozwa faini ikiwa atakutwa na hatia.

“Iwapo utapatikana na hatia, unaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka mitatu jela au faini, lakini mara nyingi faini ndio huwa uamuzi unaotolewa wakati watu wamekutwa na hatia ya matukio kama hayo.”

Wakili mwengine alisema kabla ya hukumu, lazima ufanyike uchunguzi ili mamlaka zijiridhishe kama mhusika alifanya kwa makusudi ama bahati mbaya.

“Sasa ni lazima ithibitishwe kwamba alipogonga kama alisikia sauti au aliona na akaamua kupuuzia.”

Hivi karibuni De Ligt alionekana akiwa mapumziko huko Ibiza akiwa na mkewe mwanamitindo wa Uholanzi, Annekee Molenaar.

Ikiwa itamkosa De Ligt, United imepanga kumsajili beki wa Everton, Jarrod Branthwaite ingawa itabidi timu yake ikubali kushusha bei kutoka Pauni 70 milioni wanayohitaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live