Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

De Gea mikononi mwa Al Shabab

Manchester United Wambembeleza De Gea Kurejea Old Trafford De Gea mikononi mwa Al Shabab

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Al-Shabab ya Ligi kuu soka nchini Saudi Arabia inahusishwa kuwa na mpango wa kusajili nyota kadha kutoka barani Ulaya ili kukiongezea nguvu kikosi hicho kinachoshika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Nyota wanohusishwa kujiunga na klabu hiyo ni golikipa wa zamani wa Manchester United David De Gea ambaye kwa sasa ni mchezaji huru inaripotiwa kuwa pande hizo mbili wapo kwenye mazungumzo.

Nyota wengine ni Miguel Almiron wa Newcastele united na Ivan Rakitic wa Sevilla. Na inaripotiwa kuwa Rakitic tayari amewaaga wachezaji wenzake wa Sevilla kuwa anaondoka.

Al-Shabab sio sehemu ya timu zinazoofadhiliwa na serikali ya kifalme ya Saudi Arabia kupitia mfuko wake wa kukuza michezo wa PIF (Public Investment Funs). Baadhi ya nyota wanaocheza Al-shabab ni Yannick Carrasco waingwa wa Ubeligiji na beki wa kimataifa wa Morocco Romain Saiss.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live