Kipa wa Manchester United David de Gea amesema anategemea kuwa ataendelea kusalia klabuni hapo kwa muda zaidi, akitegemea kuingia mkataba mpya.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye alijiunga na Manchester United 2011 chini ya kocha Sir Alex Ferguson, mkataba wake wa sasa unafikia ukingoni mwezi Juni.
“Nategemea kukaa hapa hadi mwisho wa taaluma yangu”, alisema. “Nimekuwa nikisema hii ni klabu yangu, nimekuwa hapa kwa muda mrefu sana”, alisema De Gea ambaye msimu huu nyavu zake hazijaguswa kwenye mechi 8 kati ya 17 ukiwa moja ya msimu wake bora.
Kwenye kipindi cha karibuni, Manchester United imekuwa na utaratibu wa kuwapa mikataba mipya wachezaji wake, Luke Shaw, Rashford, Fred na Diogo Dalot ni wachezaji walioongezewa kandarasi mpya.
De Gea, ambaye amefikisha mechi 500 ndani ya United akizungumza kumalizika kwa mkataba mpya alisema hana hofu yoyote.