Mlinda lango wa Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu nchini England Manchester United, David de Gea (32) raia wa Hispania ametwaa tuzo ya Mlinda lango bora wa EPL 2022/23 (Premier League Golden Glove).
de Gea anatwaa tuzo hiyo akiwa hajaruhusu nyavu za lango lake kutikiswa (clean sheets) katika michezo 17 akiwatangulia Allison Becker wa Liverpool na Nick Pope wa Newcastle United wakifungana kwa clean sheets 14
David de Gea ameendelea kuwa msaada mkubwa kwa United tangu alipojiunga na miamba hiyo msimu wa 2011/12 chini ya utawala wa Meneja Sir Alex Ferguson
Hata hivyo, licha ya kuendelea kutunza ubora wake langoni, lakini de Gear ameendelea kukosolewa vikali kutokana na kushindwa kuwa bora katika kuanzisha mashambulizi kwa kuwa bora katika kuchezea mpira (footwork).
Mara baada ya kila timu shiriki EPL kutimiza michezo 38 usiku wa jana, Ligi hiyo imetamatika kwa Manchester City akitwaa ubingwa huo mara pili mutawalia akiwa amekusanya alama 89.