Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

De Gea aweka rekodi ya muda wote EPL

Aston Villa V Manchester United Premier League 9 770x513 David De Gea

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Golikipa wa Manchester United David De gea ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliecheza dakika nyingi zaidi kwenye ligi kuu England (EPL) tangu kuanzishwa kwake, Hii imekuja baada ya mchezaji huyo kucheza mchezo dhidi ya Aston Villa.

Golikipa huyo aliweza kuivuka rekodi ya aliekua pia golikipa wa Manchester United Ben Forster ambae ndio alikua mchezaji anaeongoza kwa kucheza dakika nyingi kwenye ligi kuu ya England akiwa amecheza dakika 34959, Huku De gea yeye akifikisha dakika 35039 na kuivuka rekodi ya Forster.

Golikipa huyo ambae amekua kwenye kiwango bora sana kwa muda mrefu klabuni hapo ndicho kitu kilichomfanya mchezaji huyo kupata nafasi ya kucheza kwa muda mrefu na kufikisha dakika hizo, Kwani amekua akicheza karibuni michezo yote ya klabu hiyo.

David De gea ameshinda mataji yote na klabu hiyo kasoro taji la ligi ya mabingwa ulaya huku akivunja rekodi mbalimbali klabuni hapo kama vile kua golikipa wa kwanza klabuni hapo kua mchezaji bora wa msimu mara tatu mfululizo.

Licha ya kiwango hicho alichokionesha kipa huyo raia wa Hispania,lakini bado kumekua na pingamizi kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana uwezo wake hafifu wa kuweza kutumia miguu yake kwa kupiga pasi sahihi na kuanzisha mashambulizi, hivo wanahitaji golikipa mwingine mwenye uwezo wa aina hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live