Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

De Gea anachuja na utamu wake

David D Gea Slowly David De Gea

Fri, 5 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Hivi karibuni mashabiki na wachambuzi wa soka Duniani wamekuwa wakimkosoa sana kipa wa Manchester United David de Gea kutokana na makosa makubwa anayoyafanya ambayo yamekuwa yakiigharimu timu hiyo. Mbali ya kulaumiwa pia kumekuwa na tetesi kwamba Man United inaangalia uwezekano wa kusajili kipa mpya huku David Raya wa Brentford akipewa nafasi kubwa ya kutua kwa mashetani hao wekundu. Hii yote inatokana na kiwango cha De Gea cha sasa.

Lakini wakati dunia imempindukia na kumuona kwamba ni mchomaji pale Man United, de Gea ameendelea kuwa kwenye orodha ya makipa bora wa muda wote wa EPL kutokana na idadi ya mechi ambazo amecheza bila ya kuruhusu bao. Hapa tumekuletea orodha ya makipa watano ambao wamecheza mechi nyingi bila ya nyavu zao kutikiswa katika historia ya EPL na De Gea akiwa mmoja wao.

5. David Seaman - 141

Kabla ya mwaka 1992, Seaman tayari alishacheza mechi 300 za klabu akiwa na Peterborough United, Birmingham City, QPR na Arsenal. Vilevile alishashinda taji la Ligi Kuu na alishacheza mechi kadhaa za timu ya taifa ya England. Kipa huyu mafanikio makubwa aliyoyapata kwenye EPL ameshinda mataji mawili ya EPL kwenye mechi 344, pia aliwahi kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi April, 1995.

Pia kwenye michuano mingine ameshinda mataji manne ya FA , EFL Cup, ngao ya jamii mara tatu na European Cup Winners' Cup ambalo kwa sasa linaitwa Europa League. Mwaka 2002, Seaman alichukua tuzo ya golikipa bora kwa kipindi cha miaka mitano, vilevile aliweka rekodi yakuywa kipa aliyecheza mechi nyingi bila ya kufungwa kati ya mwaka 1992 hadi 2002 akifanya hivyo kwenye mechi 130.

4. Davide de Gea-145

Fundi huyu wa kimataifa wa Hispania ambaye amekuwepo kwenye Ligi Kuu England kwa zaidi ya miaka 11, amecheza jumla ya mechi 145 katika misimu tofauti tofauti na kufanikiwa kuondoka huku nyavu zake hazijatikiswa. Jumla ya mechi za EPL alizocheza hadi sasa ni 409, huku akichukua mataji nane ya michuano tofauti tofauti akiwa na mashetani hawa tangu ajiunge nao mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid.

3. Mark Schwarzer - 151

Kipa huyu kutoka Australia alicheza Ligi Kuu ya England kwa miaka 20, akipita Bradford City, Middlesbrough, Fulham, Chelsea na Leicester ambako jumla amcheza jumla ya mechi 600. Katika kipindi chote hicho staa huyu alishinda taji la EFL Cup akiwa na Middlesbrough na aliwahi kuwa mchezaji bora wa EPL kwa mwezi February, 2010.

Alicheza mechi 109 za timu ya taifa ya Australia na aliweka rekodi yakuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuichezea Chelsea akiwa na umri wa miaka 41 na siku 218, pia mchezaji mkubwa zaidi kuichezea Leicester City alipokuwa na umri wa miaka 43 na siku 32.

2. David James - 169

James aliwahi kuzichezea Liverpool, Aston Villa, West Ham, Manchester City na Portsmouth, lakini jambo la kusikitisha ni kwamba hakuwahi kupata nafasi ya kushinda taji la EPL kwenye kipindi chote alichocheza. Hata hivyo alishinda mataji ya FA Cup, EFL Cup na alicheza mechi 53 za timu ya taifa ya England.

Mechi ya mwisho ya kipa huyu kwenye EPL ilikuwa ni mwka 2010 alipokuwa anaichezea Portsmouth na hadi anastaafu alishacheza mechi 572 ambazo kwa wakati huo zilimfanya kuwa mchezaji mwenye idadi kubwa zaidi kabla ya rekodi hiyo kuvunjwa na Gareth Barry (653 ), Ryan Giggs (632), Frank Lampard (609) na James Milner (580). Lakini yeye bado anaendelea kushikilia rekodi yakuwa kipa wapili aliyecheza mechi nyingi zaidi za Ligi Kuu England bila ya kuruhusu bao.

1. Petr Cech - 202

Mwamba Huyu ndio ameweka rekodi ambayo itachukua muda mrefu hadi kuvunjwa katika historia ya Ligi Kuu England. Cech amecheza mechi 443 za ligi hii akiwa na Chelsea na Arsenal, akifanikwa kushinda mataji yote ya nchini humo, manne yakiwa ni ya EPL, matano ya FA, matatu ya EFL Cups, moja la Ligi ya Mabingwa na UEFA Super Cup moja. Mbali ya mataji Cech pia amechukua tuzo za golikipa bora wa England mara nne na anashikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi bila ya kuruhusu bao(Clean sheet) kwa msimu mmoja akifanya hivyo kwenye mechi 24. Kubwa zaidi Petr anashikilia rekodi yakuwa kipa mwenye cleen sheet nyingi zaidi tangu uanze utaratibu wa kukusanywa data kwenye ligi hiyo mwaka 1992.

Chanzo: Mwanaspoti