Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

De Gea amkataa Ronaldo, amtaka Messi

Manchester United Wambembeleza De Gea Kurejea Old Trafford De Gea amkataa Ronaldo, amtaka Messi

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa David de Gea kwa sasa hana timu na amekuwa akihusishwa sana na kurudi kwenye kikosi cha Manchester United pamoja na kwenda Saudi Arabia ambako alihusishwa na kutua Al Nassr anakokipiga Cristiano Ronaldo.

Hata hivyo, imefichuka nyota huyo amekataa ofa nono ya Pauni 500,000 kwa wiki aliyowekewa na Al Nassr na badala yake anataka kwenda kucheza soka Marekani.

Dirisha nla usajili lililopita De Gea, 33, aliwekewa ofa hiyo akaungane na Ronaldo waliowahi kukipiga pamoja Man United kabla ya Ronaldo kuondoka katikati ya msimu, huku de Gea akiachana na timu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika.

Sasa inaelezwa De Gea ameonyesha nia ya kutua Inter Miami anakocheza Lionel Messi na kupuuzia ofa hiyo ya Waarabu

Kuikataa ofa hii huenda kukazua maswali kwa mashabiki wengi huenda De Gea anamkubali Messi kuliko Ronaldo ndio maana yupo tayari kutua Marekani kwa pesa kidogo kuliko Saudia kwa pesa nyingi.

Hata hivyo, imefichuka De Gea alishindwa kukamilisha uhamisho huo kwa mujibu wa The Sun kwa sababu mkewe Edurne hapendi mazingira ya Saudia.

Kwa sasa taarifa zinadai Man United inataka kumpa ofa ya mkataba wa muda mfupi baada ya Valencia iliyodaiwa huenda ikamsajili kuwa na hali mbaya ya kiuchumi.

Hali ya maisha ya Marekani inadaiwa kumpendeza na kumvutia zaidi mke wa De Gea na inaelezwa Miami imeonyesha nia ya kutaka kumsajili lakini hawatoweza kumlipa mshahara mnono kama ule ambao Al Nassr walitaka kumpa.

Mbali ya Messi, Miami pia inawamiliki Jordi Alba na Sergio Busquets waliowahi kuwa karibu na De Gea wakati walipokuwa wakikichezea kikosi cha timu ya taifa ya Hispania.

Mwanzoni mwa mwaka ujao, Man United huenda ikakumbana na changamoto ya kutokuwa na kipa wao namba moja Andre Onana ambaye atakuwa kwenye majukumu ya kuitumikia Cameroon kwenye mashindano ya AFCON.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Januari 13 hai Februari 11, ikitegemea na hadi hatua gani Cameroon itafikia kwenye michuano hiyo.

Mbadala wa Onana kwa sasa ni Altay Bayindir aliyesajiliwa katika dirisha lililopita akitokea Fenerbahce kwa Pauni 4.3 milioni pia yupo.

Kwa sababu hii De Gea naye anaweza kusajiliwa kwa mkataba wa muda mfupi kutokana na uzoefu wake na uwezekano wa kusajiliwa kwake unaonekana kuwa mkubwa baada ya hivi karibuni kuonekana akiwa matembezini na mastaa mbali mbali wa Man United ikiwa pamoja na Sergio Reguilon na Bruno Fernandes

Chanzo: Mwanaspoti