Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

De Bruyne aweka nne, City Ubingwa ni suala la muda tu

Man City Bear Wolves Man City ni dhahiri wana nafasi kubwa ya kunyakua ubingwa wa EPL wiki chache zijazo

Thu, 12 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi, Manchester City wameitandika Wolverhampton Wanderers mabao 5-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatano Uwanja wa Molineux, Wolverhampton, West Midlands.

Nyota Mbelgiji, Kevin De Bruyne peke yake amefunga mabao manne dakika za saba. 16, 24 na 60, kabla ya Raheem Sterling kufunga la tano dakika ya 84, wakati la Wolves limefungwa na Leander Dendoncker dakika ya 11.

Man City imefikisha pointi 89, tatu zaidi ya Liverpool baada ya wote kucheza mechi 36.

Wolves wanabaki na pointi zao 50 za mechi 36 pia nafasi ya nane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live