Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

De Bruyne ausuuza moyo wa Guardiola

De Bruyne 1140x640 De Bruyne ausuuza moyo wa Guardiola

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Klabu Bingwa Duniani Man City, Pep Guardiola amemsifia kiungo Kevin de Bruyne kuwa ni kipenzi cha wengi baada ya kucheza mechi ya kwanza msimu huu mwishoni juma lililopita.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa Kombe la FA, Man City iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Huddersfield, De Bruyne aliingia katika dakika ya 57 kuchukua nafasi ya Julien Alvarez.

Umati mkubwa wa mashabiki waliokuwa katika Uwanja wa Etihad ulisimama kumshangilia De Bruyne ambaye hakuwa amecheza tangu Agosti 11, mwaka jana jambo lililomfanya Guardiola ampongeze akisemani wa kipekee.

“Kevin anatakiwa kufahamu ni kwa kiasi gani watu wanampenda. Ni wa aina yake. Hadi atakapoamua kuondoka au kustaafu atabakia milele kuwa miongonu mwa wachezaji wanaopendwa zaidi,” amesema Guardiola.

Licha ya kukaa nje kwa muda mrefu, De Bruyne alionyesha ubora kwa kupika bao la nne.

Chanzo: Dar24