Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

De Bruyne atupia bao 2 Man City ikishinda 4-2

IMG 6670.jpeg Kevin De Bruyne

Sun, 7 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Mbelgiji, Kevin De Bruyne amefunga mabao mawili kuiwezesha Manchester City kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wenyeji, Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Jana Jumamosi Uwanja wa Venue Selhurst Park Jijini London.

Kevin De Bruyne (32) amefunga mabao yake dakika ya 13 na 70, huku mabao mengine ya mabingwa hao watetezi yakifungwa na kinda wa miaka 19 wa England, Rico Lewis dakika ya 47 na mshambuliaji Mnorway, Erling Haaland dakika ya 66.

Kwa upande wao Crystal Palace mabao yao yamefungwa na washambuliaji Wafaransa, Jean-Philippe Mateta dakika ya tatu na Odsonne Édouard dakika ya 86.

Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 70 katika mchezo wa 31 na kuendela kubaki nafasi ya tatu nyuma ya vinara Arsenal na Liverpool.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live