Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

De Bruyne apata leseni ya ukocha

Kvin De Bruyneeeeee Kevin De Bruyne

Wed, 1 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin De Bruyne alikuwa miongoni mwa wachezaji 18 wa kimataifa wa sasa na wa zamani wa Ubelgiji walipewa leseni zao za ukocha Jana baada ya kufanya kozi ya miaka miwili na Shirikisho la Soka nchini la Ubelgiji (RBFA).

Wachezaji wengi walipewa leseni za ukocha ni mshambuliaji wa Napoli Dries Mertens, mlinzi wa Benfica Jan Vertonghen, Axel Witsel wa Borussia Dortmund na wachezaji wawili wa Leicester City Youri Tielemans na Dennis Praet.

Mkufunzi mkuu wa makocha Kris Van Der Haegen, alisema wazo la kuwafundisha wachezaji hao ukocha ni kuwaweka tayari kujua wanachokitaka baada ya Kustaafu soka.

Beki wa zamani wa Arsenal Thomas Vermaelen aliyestaafu mwaka jana na kwa sasa ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ni sehemu ya mafaniko ya mpango huu. Kuna cha kujifunza hapa, Usisubiri kumekucha ndio utafute shuka la kijifunika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live