Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

De Bruyne afanya makubaliano na Ittihad

KDB KDB De Bruyne afanya makubaliano na Ittihad

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne ameripotiwa kufikia makubaliano binafsi na Al Ittihad ya Saudi Arabia ambayo atajiunga nayo katika dirisha hili.

Staa huuu mwenye umri wa miaka 33, amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na amekuwa akihusishwa na timu za Saudia tangu mwaka jana.

Inaelezwa kocha mpya wa Ittihad, Laurent Blanc ndio amesisitiza kwamba anahitaji huduma ya De Bruyne katika kikosi chake ambacho tayari kina mastaa kama N'Golo Kante na Karim Benzema.

Man City ipo tayari kumuuza staa huyu ili asije kuondoka bure mwisho wa msimu ujao na inaelezwa inaweza kumwachia kwa zaidi ya Pauni 40 milioni.

Ittihad imeripotiwa kumwekea mezani kiungo huyu ofa nono ya mshahara unaofikia Pauni 1 milioni kwa wiki.

Msimu uliopita hakupata muda mwingi wa kucheza kutokana na majeraha ya mara kwa mara yaliyokuwa yanamwandama.

Wakati huo huo Manchester United imeripotiwa kuwa tayari kumuuza kiungo wao Mason Mount katika diriisha hili baada ya kocha wao Erik ten Hag kutiridhishwa na kiwango alichoonyesha tangu ajiunge nao katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana.

Mount mwenye umri wa miaka 25, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, kwa sasa yuko katika maandalizi ya msimu na Man United.

ARSENAL ipo katika hatua za mwisho kumsajili kipa wa Ajax, Tommy Setford latika dirisha hili kabla ya kwenda Marekani watakakoweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu.

Setford ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwakani. Msimu uliopita alicheza mechi 15 za michuano yote.

MABOSI wa Arsenal wamezidisha nguvu ktika harakati zao za kuiwania saini ya beki wa Bologna na Italia Riccardo Calafiori, 22, ambaye imeripotiwa kufanya naye makubaliano binafsi lakini kinachomwamisha dili ni kiasi cha pesa kinachohitajika na Bologna ili kumuuza.

Mkataba wa sasa wa staa huyu unamalizika mwaka 2027. Msimu uliopita alicheza mechi 37 za michuano yote.

WEST Ham imefanya makubaliano kwa njia ya mazungumzo na kiungo wa Al Ittihad na Ufaransa, N'Golo Kante, 33, kwa ajili ya kumsajili katika dirisha hili.

West Ham imekuwa ikipambana tangu wiki iliyopita na taarifa kutoka The Athletic zinaeleza kwa sasa wamefikia katika hatua nzuri. Mkataba wa Kante na Ittihad unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.

MANCHESTER United bado inaendelea kufanya mazungumzo na mabosi wa Paris St-Germain juu ya kiungo wa timi hiyo na Uruguay, Manuel Ugarte, 23, kwa ajili ya kumsajili katika dirisha hili.

Ripoti zinaeleza tayari mashetano hao wekundu wameshafanya makubaliano na upande wa mchezaji mwenyewe na kilichobakia ni kumalizana na PSG, inayodaiwa kuhitaji zaidi ya Pauni 30 milioni.

MANCHESTER United inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 30 milioni kutoka kwa timu itakayohitaji saini ya kiungo wao raia wa Scotland, Scott McTominay, 27, katika dirisha hili.

Scott ni miongoni mwa wachezaji ambao mabosi wa Man United wanataka kuwauza katika dirisha hili kwa ajili ya kukusanya pesa itakazotumia kufanyia usajili. Mkataba wake unamalizika mwaka 2025.

BRIGHTON imefanya mazungumzo na Inter Miami juu ya mpango wa kumsajili kiungo wa timu hiyo na Paraguay, Diego Gomez ambaye alionyesha kiwango bora akiwa na Miami kwa msimu uliopita, vilevile katika michuano ya Copa America akiwa na taifa lake.

Gomez mwenye umri wa miaka 21, mkataba wake unamalizika mwaka 2026.

Chanzo: Mwanaspoti