Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

De Bruyne: Timu yetu ina wazee haiwezi shinda Kombe la Dunia

Belgium Kikosi cha Timu ya Taifa ya Ubelgiji

Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kupokea kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa Morocco, Kiungo wa Kimataifa wa Ubelgiji anayekipiga Man City, Kevin De Bryune haamini kama Timu ya Taifa ya Ubelgiji inaweza kubeba kombe la Dunia linaloendelea nchini Qatar.

De Bruyne ametoa kauli hiyo akiamini kuwa uwezo wa kikosi chao umepungua kutokana na wachezaji wengi wa kikosi hicho kuwa na umri mkubwa.

"2018 tulikuwa na nafasi ya kushinda kombe la Dunia ingawa hatukufanikiwa, Msimu huu siioni nafasi ya kushinda ubingwa kwa sababu asilimia kubwa ya wachezaji wa timu yetu ni wazee na mashindano yana kasi sana " amesema kiungo huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live