Kevin De Bruyne mchezaji bora wa Premier League 2022 amefurahia kufanya kazi na usajili mpya wa Man City Erling Haaland na amekiri ujio wa fowadi huyo utaboresha sana safu ya ushmabuliaji na kumpa wigo mpana wa kutoa asisti.
Licha ya kuwa na msimu mzuri wa kufunga mabao De Bruyne alishindwa kuwa na idadi kubwa ya kusaidia mabao hivyo anaamini uwepo wa Haaland utasaidia kuweka asisti nyingi.
Haaland ameondoka Dortmund akiwa amefunga jumla ya mabao 86 katika michezo 89 tangu ajiunge na klabu hiyo ya Ujerumani akitokea Sallzburg mwaka 2020 na anatarajia kuungana na De Bruyne ambaye inaaminika atamsadia katika pasi za mwiosho.
Akizungumza na HLN, De Bruyne alisema kuwa ujio wa Haaland ulikuwa habari njema kwa timu na yeye mwenyewe.
“Erling Haaland ni mshambuliaji wa juu. Hatua yake inapaswa kutusaidia kukua kama timu,” alisema.
“Kila mtu anatarajia mengi. klabu daima imekuwa ikitafuta namba tisa, lakini nadhani itakuwa vizuri kuwa na mshambuliaji huyo ambaye labda anafunga mabao 20 hadi 25 kwa msimu.”