Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Davies aweka rekodi, Canada safari imewakuta

Alphonso 640x360 Davies aweka rekodi, Canada safari imewakuta

Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Alphonso Davies ameweka rekodi yake ya kuwa nyota wa kwanza kufunga bao la mapema zaidi kwenye Kombe la Dunia Qatar 2022.

Ilikuwa dakika ya 2 alipachika bao hilo lakini halikutosha kuipa pointi tatu timu yake kwa kuwa baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Khalifa ulisoma Croatia 4-1 Canada.

Kwenye kundi F, Canada imetolewa kwenye mashindano kwa kuwa haina pointi na mchezo wake wa mwisho ni dhidi ya Morocco wenye pointi nne sawa na Croatia unatarajiwa kuchezwa Desemba Mosi.

Ni mabao ya Anres Lramaric aliyepachika mabao mawili dakika ya 36 na 70 kisha moja ni mali ya Marco Livaja dakika ya 44 na bao la nne alipachika Lovro Majer.

Pia Ubelgiji wao watasaka ushindi mbele ya Croatia kwenye kusaka tiketi ya kufuzu 16 bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live