Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

David Raya ashinda Tuzo ya Golden Glove

David Ray Golden David Raya

Sat, 4 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyanda wa klabu ya Arsenal, David Raya ametwaa tuzo ya Glavu ya dhahabu (Golden glove) kama Golikipa mwenye mechi nyingi bila kuruhusu bao ‘clean sheet’ kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Hii ni baada ya golikipa wa Everton Jordan Pickford kuruhusu goli dhidi ya Luton na kumfanya ashindwe kumpiku ingawa anaweza kumfikia ikiwa atapata ‘clean sheets’ kwenye mechi mbili za Everton zilizosalia kabla ya kufungwa kwa pazia la Ligi hiyo.

MSIMAMO WA CLEAN SHEETS EPL HADI SASA

14—David Raya (Arsenal)

12—Jordan Pickford (Everton)

9—Bernd Leno (Fulham)

9—Ederson (Man City)

Raya anakuwa golikipa wa kwanza wa Arsenal kutwaa ‘Golden glove’ tangu Petr Cech alipofanya hivyo msimu wa 2015/16.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live