Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

David Raya afichua siri nzito Arsenal

David Raya David Raya afichua siri nzito Arsenal

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: Dar24

Mlinda Lango mpya wa Arsenal, David Raya ameweka wazi angekufurahi zaidi kama angekua anacheza nafasi tofauti badala ya kipa ambayo anaicheza kwa sasa.

Kipa huyo alitoboa siri hiyo kufuatia uhamisho wake wa kujiunga na Arsenal kwa mkopo akitokea Brentford iliyogharimu Pauni 13 milioni na kipengele cha kununuliwa jumla kwa Pauni 27 milioni endapo kiwango chake kitamshawishi Mikel Arteta.

Raya alisema awali alikuwa akicheza nafasi nyingine kabla ya kuwa kipa na kushinikizwa na ndugu yake kuwa kipa.

Kipa huyo wa kimataifa wa Hispania alianza kuichezea Southport kwa mkopo kuanzia msimu wa 2014-2015 kabla ya Brentford kumsajili mwaka 2019.

Na kutokana na ubora wake alioonyesha msimu uliopita aliisaidia Brentford kumaliza msimu katika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Baada ya kukamilsha uhamisho wa kujiunga na Arsenal kipa huyo aliwaambia waandishi wa habari wa Brentford: “Nilivyokuwa Hispania nilicheza Ligi Daraja la Tatu kama mchezaji wa kawaida na sio kipa.

Baadaye akaelezea kwa kina kupitia tovuti ya Arsenal: “Kaka yangu alipenda kuniweka golini, lakini nikicheza na marafiki zangu siku zote napenda kucheza nafasi tofauti kabisa. Nafurahia kucheza nafasi tofauti kabisa ndio maana najiamini nikiwa na mpira mguuni,” alisema Raya ambaye atakuwa na upinzani na Aaron Ramsdale.

Chanzo: Dar24