Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

David Raya: Sina tatizo na Ramsdale

Arsenal Goalkeepers Aaron Ramsdale David Raya David Raya: Sina tatizo na Ramsdale

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Golikipa Mhispaniola ambaye ameanza kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Mikel Arteta, David Raya ameelezea mahusiano yake na kipa namba moja wa Arsenal, Aaron Ramsdale tangu ameanza kucheza na kubainisha kuwa wana mahusiano mazuri baina yao.

Raya aliulizwa swali akasema mahusiano yetu?

" Tuna mahusiano mazuri mimi na Ramsdale, na jambo zuri pia tumekuwa tukisaidiana hata mazoezi, wakati ambao Ramsdale hana nyakati nzuri namsaidia namimi nikiwa nipo chini anafanya hivyo pia. Ndiyo ushirikiano unaotakiwa eneo la ulinzi, bila hivyo mazoezi hayawezi kwenda vizuri.

Raya aliongeza kuwa, Namshukuru Arteta amenipa ujasiri na kujiamini kukaa langoni na ndiyo kitu nilikuwa nakihitaji, hata yeye amekuwa akisema anahitaji wachezaji wazuri kwenye kila eneo."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live