Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

David De Gea afikisha michezo 400 EPL

David De Gea !!.jpeg David De Gea

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Golikipa wa klabu ya Manchester United David De Gea raia wa Hispania amefanikiwa kuweka rekodi ya kua mchezaji wa kwanza asiye raia wa Uingereza kucheza michezo 400 ya ligi kuu ya England.

Golikipa De Gea ambaye mpaka sasa anaitumikia klabu ya Manchester United ndani ya msimu wake wa 12 tangu amejiunga ndani ya klabu hiyo mwaka 2011, Kipa huyo amefanikiwa kuweka rekodi hiyo baada ya kuanza katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Leeds United.

Goliklipa huyo ambaye ni mchezaji pekee ambaye anapata nafasi kwenye timu hiyo ambaye alikua kikosi cha Sir Alex Ferguson mwaka 2013, Hii inaonesha kua ni mchezaji ambaye ameonesha ubora wake kwa muda mrefu ndani ya klabu hiyo.

David De Gea amefanikiwa kubeba mataji yote ndani ya timu hiyo kasoro taji la ligi ya mabingwa ulaya, Kwani golikipa huyo kashinda mataji kama ligi kuu ya Uingereza, Fa Cup, Carabao Cup, pamoja na kombe la Europe League na kua mchezaji pekee alieshinda taji la ligi kuu ya Uingereza ndani kikosi hicho kwasasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live