Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

David Brayson ageuka dili Dirisha la usajili

Bryson Yanga' David Bryson ( kulia)

Sun, 25 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa KMC umeanza mazungumzo ya kimya kimya ya kumrejesha aliyekuwa beki wa kushoto wa timu hiyo, David Bryson ambaye mkataba wake aliosaini wa miaka miwili na Yanga unafikia tamati msimu huu.

Nyota huyo alijiunga na Yanga Agosti 2021 akitokea KMC ambako alionyesha kiwango kizuri na kuzivutia timu nyingi ingawa tangu amejiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara mambo yamekuwa ni magumu.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo kililiambia Mwanaspoti, Bryson licha ya kutopata nafasi ya kucheza ila bado ni mchezaji mzuri na anaweza kujiunga nao kama mambo yataenda sawia.

"Tunatarajia kukutana hivi karibuni kujadili mambo mbalimbali ya timu kwa ajili ya msimu ujao, suala la Bryson siwezi kusema ni kweli au laah! hivyo tusubirie kwanza," kilisema chanzo hicho.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Jamhuri Kihwelo 'Julio' alisema tayari alishakamilisha ripoti yake kwa ajili ya msimu ujao na kazi iliyobaki ni kwa viongozi kumtimizia mahitaji yake.

Awali Mwanaspoti ilipofanya mahojiano na Mkurugenzi Mtendaji wa timu hiyo, Daniel Mwakasungula alisema walikutana jana kujadili msimu mzima ulivyokuwa ikiwemo usajili mpya na hatima ya kocha wao.

Hatma ya Julio inakuja baada ya kocha huyo aliyechukua nafasi ya Mnyarwanda, Theirry Hitimana aliyetimuliwa na wasaidizi wake mapema Aprili mwaka huu kupewa kandarasi ya miezi mitatu tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: