Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dar, Mbeya zapishana hatua ya makundi CRDB Bank Taifa Cup

Kikapu Pic Data Dar, Mbeya zapishana hatua ya makundi CRDB Bank Taifa Cup

Fri, 29 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. Timu za Mbeya na Dar es Salaam zinazotajwa kuwa miongoni mwa zitakazoonyesha upinzani kwenye mashindano ya mpira wa kikapu ya taifa maarufu kama CRDB Bank Taifa Cup yatakayofanyika kwa siku 10 kuanzia Novemba 5 jijini Dodoma zimepishana kwenye hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Droo ya makundi imepangwa hii leo huku wadhamini wa mashindano hayo, benki ya CRDB ikibainisha kukamilisha maandalizi kwa asilimia 90 na kilichobaki ni timu kuonyesha ushindani.

Bingwa mtetezi, Mbeya ambayo imetamba kutetea ubingwa huo imepangwa kundi C na timu za CRDB Youth, Iringa, Tabora na Manyara.

Wakati vigogo Dar es Salaam 'Dream team' ambao wana ndoto ya kurejesha heshima yao kwenye mashindano hayo wao wako kundi B na timu za Pemba, Shinyanga, Pwani na Kigoma.

Kwenye kundi A kuna timu za Mwanza, Mtwara, Rukwa, Kilimanjaro na Unguja huku kundi D likiwa na wenyeji Dodoma, Simiyu, Tanga, Arusha na Morogoro.

Kwa wanawake, Dodoma, Mtwara, Unguja na Iringa zimepangwa kundi A, wakati Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na CRDB Youth zikiwa kundi B na Pemba, Tanga, Mbeya na Pwani zenyewe zimeangukia kundi C.

"Hii inaashiria picha ya ushindani sasa imeanza," amesema Kilo Mgaya meneja uhusiano wa benki ya CRDB.

Kamishina wa wanawake wa Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF), Agnela Semwaiko amesema kwa ratiba hiyo ya makundi ni wakati wa timu kufanya skauti kuwafahamu wapinzani wao na kujipanga ili kufanya vizuri.

Tofauti na msimu mingine, msimu huu hamasa ni kubwa na ushindani utakuwa mkali hasa kwenye mechi za kundi B kwa wanawake na kundi B na C kwa wanaume," amesema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz