Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dante kuikosa Singida Big Stars

Dante Pic Data Beki wa KMC, Andrew Vicent

Mon, 1 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Hii inaweza kuwa habari njema kwa Singida Big Stars lakini ni mbaya kwa klabu ya KMC baada ya beki wao kisiki, Andrew Vicent 'Dante' kutokuwa sehemu ya mchezo wa Ligi Kuu pindi timu hizo zitakapokutana. KMC itaikaribisha Singida BS, Mei 12 mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni.

Katika mchezo huo KMC itamkosa beki wake kisiki, Dante ambaye ana kadi tatu za njano alizozipata kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar, Tanzania Prisons na Dodoma Jiji.

Kukosekana kwa Dante itawalazimu benchi la ufundi kumuanzisha Ibrahim Ame na Ismail Gambo ambaye alicheza sambamba na Dante katika mchezo wao uliopita dhidi ya Dodoma Jiji.

Ame na yeye itaangaliwa hali yake kwa sababu inaelezwa kwamba mchezaji huyo anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja na ndio maana alikosa mchezo uliopita.

Kama Ame bado hayupo fiti basi Sadala Lipangile ambaye awali alikuwa anacheza kama mshambuliaji wa kati ni mzuri kwenye kucheza kama beki na alishafanya hivyo kwenye misimu kadhaa nyuma.

Mwanaspoti linafahamu kwamba Dante hayupo sehemu ya kikosi kinachoendelea na maandalizi ya mechi yao ijayo dhidi ya Singida Bs.

Chanzo kutoka ndani ya timu hiyo kililidokeza Mwanaspoti kikisema;"Kila kitu kinawezekana na benchi letu la ufundi linaendelea na maandalizi, muda bado upo wa kutengeneza kikosi hasa kwenye eneo la ulinzi."

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: