Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dante aichimba mkwara Yanga kimtindo

Dante Pic Data Beki wa KMC, Andrew Vicent

Sat, 9 Oct 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Beki Andrew Vicent 'Dante' anayecheza katika klabu ya KMC amesema anatambua ugumu wa mchezo wao ujao dhidi ya Yanga lakini wamejipanga kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

KMC itaikaribisha Yanga kwenye uwanja wa Majimaji Songea, mchezo utakaopigwa Oktoba 19.

Dante amesema ugumu wa mchezo huo unatokana na wao kuanza vibaya msimu na wanahitaji matokeo mazuri huku pia wapinzani wao wakitaka kuendeleza ushindi ambao wanao.

"Tulifanya vibaya kwenye mechi zilizopita na tunahitaji ushindi kwenye mchezo huu, Yanga najua watataka kupata matokeo kwa sababu wanautaka ubingwa kama wanavyosema hivyo mchezo lazima uwe mgumu," alisema Dante.

Mechi ya Yanga na KMC imekuwa na vuta ni kuvute huku msimu uliopita mchezo wao wa kwanza walitoka sare 1-1 bao la KMC likifungwa na David Bryson na upande wa Yanga likifungwa na Yacouba Sogne.

Kwenye mechi ya pili Yanga ilishinda 2-1 bao la KMC likifungwa na Hassan Kabunda na mabao ya Yanga yalifungwa na Tuisila Kisinda (Penalti) kisha Waziri Junior alifunga bao la ushindi.

Chanzo: Mwanaspoti