Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dante, Vicent Aboubakar kukikosa KMC leo

Dante Pic Data Beki wa kati wa KMC FC, Andrew Vincent ‘Dante’

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya KMC imethibitisha kuwakosa wachezaji wake Andrew Vicent Dante na Vicent Aboubakar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

KMC imetaja sababu mastaa hao kuukosa mchezo huo utakaochezwa jioni ya leo kuwa ni majeruhi.

Yanga itashuka dimbani hii leo ikiwa ni mchezo wa ufunguzi wa ligi kwa msimu wa 2023/2024 baada ya kuchelewa kutokana na mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya ASAS ya Djibou iliyoibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Huu utakuwa mchezo wa pili kwa KMC baada ya ule wa kwanza kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: