Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daniel Mgore akaribia kutua Dodoma Jiji FC

Mgore.png Mlinda Mlango Daniel Mgore

Thu, 7 Jul 2022 Chanzo: dar24.com

Klabu ya Dodoma Jiji FC, ipo mbioni kukamilisha usajili wa Mlinda Mlango Daniel Mgore kutoka Biashara United Mara, iliyoshuka Daraja kutoka Ligi Kuu hadi Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2022/23.

Dodoma FC inaendelea na mchakato wa kukiboresha kikosi chake katika kipindi hiki cha Dirisha la Usajili, huku ikiwa imeshakamilisha usajili wa baadhi ya wachezaji kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Jana Jumatano (Julai 06), Klabu hiyo ya mjini Dodoma ilikamilisha usajili wa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Collins Opare, akitokea Biashara United Mara.

Endapo Mgore atakamilisha dili la kujiunga na klabu hiyo, atakuwa mchezaji wa pili aliyesajiliwa kutoka Biashara United Mara, ambayo inaendelea kupunguzwa nguvu, kutokana na zuio la kufungiwa kusajili kutoka FIFA.

Mgore ambaye ni Raia wa Tanzania ni miongoni mwa Walinda Lango ambao wamekuwa wakifanya vyema sana kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

Chanzo: dar24.com