Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dani Olmo atakiwa England

Dani Olmo Dani Olmo

Mon, 10 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United, Manchester City, Liverpool bado hazijakata tamaa kwenye vita ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa RB Leipzig, Dani Olmo katika dirisha hili licha ya Bayern Munich kuonekana ipo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumpata.

Olmo mwenye umri wa miaka 26, anawindwa na timu nyingi kutokana na kiwango bora alichoonyesha msimu uliomalizika.

Tanguy Ndombele

KIUNGO wa Tottenham, Mfaransa Tanguy Ndombele, 27, anatarajiwa kuondoka akiwa huru katika dirisha hili ambapo mkataba wake utakuwa unamalizika.

Ndombele ambaye hakuwa anapata nafasi kubwa ya kucheza kwa msimu uliopita hayupo kwenye mipango ya benchi la ufundi la Spurs kwa msimu ujao kiasi cha kuamua kutomuongeza mkataba.

Amadou Onana

KIUNGO wa Everton na Ubelgiji, Amadou Onana ameweka wazi kuwa anafikiria kujiunga na moja kati ya timu kubwa barani Ulaya itakayokuwa inashiriki michuano ya kimataifa.

Staa huyu ambaye anahusishwa na Arsenal huenda akauzwa kwa zaidi ya Pauni 50 milioni.

Amekuwa akiwindwa na timu nyingi barani Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu msimu uliopita.

Christopher Nkunku

CHELSEA imepokea ofa kutoka timu kadhaa zinazohitaji huduma ya mshambuliaji wao Christopher Nkunku, katika dirisha hili lakini mchezaji mwenyewe amegoma kuondoka kwani bado anaamini ana nafasi kwenye timu hiyo.

Nkuku ambaye tangu atue Chelsea katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana amekiwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara, mkataba wake unamalizika mwaka 2029.

Giovani Lo Celso

REAL Betis inataka kumsajili kiungo wa Tottenham na Argentina, Giovani Lo Celso katika dirisha hili.

Mabosi wa Betis wamepata matumaini ya kumsajili kiungo huyu kwa sababu haonekani kuwa kwenye mipango ya benchi la ufundi la Spurs kuelekea msimu ujao.

Lo Celso kutoka Argentina anataka kuhakikishiwa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza kwa timu itakayohitaji kumsajili.

Arne Slot

KOCHA mpya wa Liverpool, Arne Slot amependekeza jina la winga wa Newcastle United ambaye msimu uliomalizika alikuwa akicheza kwa mkopo Feynoord ambako alimfundisha.

Hata hivyo, Newcastle inadaiwa kuwa haina mpango wa kumuuza staa huyo wa kimataifa wa Gambia kwa sasa na hata kama ikitokea ikamuuza itahitaji zaidi ya Pauni 30 milioni.

Joshua Zirkzee

AC Milan imeshaanza mazungumzo na wawakilishi wa straika wa Bologna Joshua Zirkzee ili kumpata katika dirisha hili.

Taarifa za wiki iliyopita zilifichua kwamba straika huyu na wawakilishi wake wapo jijini London

kwa ajili ya kufanya mazungumzo na baadhi ya timu zilizoonyesha nia ya kutaka kumsajili katika dirisha hili.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna timu yoyote ya England liyofikia makubaliano ya kumsajili ingawa mazungumzo bado yanaendelea.

Chanzo: Mwanaspoti