Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dani Alves mali alizoacha uraiani

Alves Stle Dani Alves mali alizoacha uraiani

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wiki iliyopita mchezaji wa zamani wa Barcelona, Dani Alves alikutwa na hatia ya kufanya unyanyasaji wa kijinsia kwa mwanamke mmoja huko jijini Barcelona nchini Hispania ambako mahakama nchini humo imemhukumu kifungo jela cha miaka minne na nusu.

Mbali ya hukumu hiyo pia Alves ametakiwa kumlipa fidia ya Pauni 130,000 muathirika wa tukio hilo, huku staa mwenzake wa Brazil, Neymar akiahidi kumlipia kiasi hicho cha pesa.

Staa huyu alifanya tukio hili Desemba 30, 2022 katika moja ya kumbi za starehe huko nchini Hispania mida ya usiku.

Wakili wake amesema kwamba watakatia rufaa hukumu hiyo na wanaamini Alves hana hatia. Kwa mujibu wa Daily Mail, akaunti ya staa huyu kwa sasa inasoma anadaiwa Pauni 17,000 (sawa na Sh54.7 milioni. Jamaa amebaki na mali kibao uraiani ikiwa pamoja na nyumba na magari. Hapa tumekusogezea jinsi jamaa alivyowahi kupiga pesa na vitu ambavyo ameviacha uraiani.

ALIPIGAJE PESA

Mwaka 2013, Barcelona alipokuwa anajiunga na Barcelona alikuwa akipewa mshahara wa Dola 9 milioni kwa mwaka ambayo iliongezeka kufikia Dola 9.1 milioni kwa mwaka wa pili.

Alipojiunga na Juventus alikuwa akichukua Dola 4.54 milioni kwa mwaka na alicheza hapo kwa mwaka mmoja, ilipofika mwaka 2017 alijiunga na Paris Saint-Germain ambako alikuwa akichukua mshahara wa Euro 700,000 (Pauni 597,928) kwa mwezi iliyokuwa sawa na Pauni 160,000 kwa wiki.

Baada ya kuzikusanya pesa za kutosha kwenye soka la ushindani aliamua kwenda kupumzisha akili nchini kwao Brazil alipojiunga na Sao Paulo kabla ya kurejea tena Barcelona ambako ripoti zinadai alikuwa akipata mshahara wa Pauni 5000 kwa wiki ambao ni zaidi na milioni 15 za Kitanzania, akiwa ndio mchezaji aliyekuwa akilipwa kiasi kidogo zaidi kwenye kikosi cha kwanza cha Barca kwa wakati huo. Alifanya hivyo kwa mapenzi yake ya timu hiyo akisema hakwenda kusaka pesa. Alitaka tu kuisaidia timu iliyompa utajiri na mafanikio ya makombe mengi.

Alipojiunga na UNAM ya Mexico mwaka 2022, alikuwa akilipwa kiasi kisichopungua Euro 6 milioni kwa mwaka.

Mbali ya pesa alizokusanya kupitia mishahara na pesa za usajili. Jamaa pia alikuwa na madili ya udhamini na kampuni mbalimbali kama Nike na EA Sports.

Pia anamiliki nyumba kibao huko nchini Brazil ambazo anazipangisha pia ana migahawa nchini humo.

MAGARI

Audi RS6 Dola 245,116

Audi Q7 Dola 49,950,

Audi RS6 Avant C7 Dola 700,000,

Ferrari FF Dola 3.6 milioni

Volvo C30 T5 Dola 500,00,

Mercedes Benz Dola 549,80.

NYUMBA

Ukiacha nyumba za biashara nchini kwao, jamaa alikuwa na nyumba tatu katika nchi tofauti, mjengo wa kwanza ni ule wa nchini Hispania ambao aliuuza baada ya kuondoka Barcelona lakini mbali ya hiyo kwa sasa anamiliki nyumba nyingine mbili moja ikiwa kule Paris Ufaransa na ile ya Juazeiro huko nchini kwao Brazil.

MSAADA KWA JAMII

Jamaa amekuwa mmoja kati ya wadau wakubwa wa kutoa misaada kwenye taasisi mbalimbali na mara kadhaa amekuwa akijumuika kwenye vituo vya watoto yatima kwa ajili ya kula chakula cha jioni na watoto hao. Pia kwa mwaka amekuwa akisaidia watu wasiopungua 10 kufanyiwa upasuaji wa moyo.

MAISHA NA BATA

Licha ya timu yake ya mwisho UNAM ya Mexico, kuwahi kumlipa Euro 6 milioni kwa mwaka, staa huyu anadaiwa kwa sasa hana pesa kabisa kwenye zake kutokana na maisha ya starehe aliyokuwa akiishi.

Aliwahi kuwa kwenye ndoa na mrembo Joana Sanz ambaye walioana mwaka 2017 lakini kabla ya hapo aliwahi kumuoa Dinora Santana mwaka 2008 na akaachana naye mwaka 2011.

Santana ndio alibahatika kupata naye watoto wawili ambao ni Victoria Alves na Daniel Alves.

Chanzo: Mwanaspoti