Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dani Alves kupandishwa kizimbani tuhuma za Ubakaji

Dani Alves Pp Beki wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Dani Alves

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Dani Alves atatinga mahakamani Hispania kujibu mashtaka ya tuhuma za unyanyasaji wa kingono kwa mwanamke mmoja katika klabu iliyopo Barcelona Disemba mwaka jana taarifa imethibitshwa.

Alves mwenye umri wa 40 alikamatwa Januari 20 na kusota jela iliyopo nje ya Barcelona. Iwapo atapatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka minne hadi 15 jela. Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Brazil, ambaye pia aliwahi kuzichezea Sevilla, Juventus na PSG, amekana kufanya makosa hayo.

Katika hati iliyosainiwa na majaji watatu, mahakama ya upelelezi namba 15 huko Barcelona, ilisema kuna sababu za kutosha kwa Alves kujibu mashtaka, kufuatia maombi ya mwendesha mashtaka wa umma na mwanamke huyo.

Chini ya sheria ya ridhaa masuala ya kijinsia huko Hispania iliyopitishwa mwaka jana unyanyasaji wa kijinsia unachukua nafasi kubwa kwani ni uhalifu ambao haukubaliki kwenye jamii.

Alves alisema hapo awali baada ya kukamatawa: “Itathibitishwa kuwa sina hatia na yalikuwa mahusiano ya makubaliano. Haiingii akilini eti nimelazimisha tendo la ndoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live