Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dani Alves bado yupo kwenye nondo

Dani Alves Pp Dani Alves bado yupo kwenye nondo

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama mjini Barcelona inayoshughulikia kesi dhidi ya mchezaji soka Dani Alves, ilifanya kikao Alhamisi ambapo upande wa mashtaka na utetezi uliwasilisha hoja zao kuhusu rufaa iliyokatwa na mchezaji huyo wa zamani wa Barca, PSG na Juventus kupinga uamuzi wa mahakama kumweka rumande kwa tuhuma za ubakaji.

Alves anatuhumiwa kumbaka binti katika kilabu ya usiku katika mji mkuu wa Kikatalani.

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Umma na upande wa mashtaka wameomba kwamba Alves abaki katika kizuizi wakisema yuko kwenye hatari ya kukimbia na kupoteza ushahidi dhidi yake.

Kikosi cha mawakili cha Alves, kikiongozwa na Cristóbal Martell, ambaye alimwakilisha Lionel Messi wakati wa kesi ya ulaghai wa kodi, walisema kwamba kwa vile mwathirika hakupata majeraha yoyote katika sehemu zake za siri kitendo hicho kilikuwa cha makubaliano.

Kwa hivyo, upande wa utetezi sasa unadhani kuwa mlalamikaji aliingiliwa tukio ambalo Alves alikanusha awali katika maelezo yake mahakamani.

Uchunguzi wa kibaolojia umebaini kuwa mwanamke huyo alikuwa na chembechembe za mbegu za kiume katika sehemu yake ya siri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live