Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dani Alves atupwa jela kwa unyanyasaji wa kingono

Dani Alves Kufungwa Miaka 12 Jela Dani Alves

Thu, 22 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na Klabu ya Barcelona, Dani Alves amehukumiwa kwenda jela miaka minne na nusu mara baada ya kukutwa na hatia ya kosa la unyanyasaji wa kingono kwa Mwanamke mmoja kwenye Club ya usiku katika jiji la Barcelona.

Mahakama hiyo chini ya Jopo la majaji watatu leo Februari 21 limemhukumu Alves kifungo cha miaka minne na miezi sita jela uamuzi ambao unaweza kukatiwa rufaa.

Hata hivyo Alves, mwenye umri wa miaka 40, amekana kuhusika na kosa lolote katika kesi hiyo iliyoendeshwa kwa muda wa siku tatu mwezi huu.

Alves ambaye amekua rumande tangu mwaka 2023 akisubiri hukumu hii, ametakiwa pia kumlipa fidia ya euro 150,000 (Tsh milioni 414) Mwanamke huyo.

Je, unadhani ni kipi kinawapelekea Wachezaji wengi kuhukumiwa na makosa ya unyanyasaji wa kingono?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live