Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dani Alves akutwa na hatia ya ubakaji, atupwa jela miaka 4

Dani Alves Akutwa Na Hatia Ya Kumbaka Mwanamke Klabu Dani Alves akutwa na hatia ya ubakaji, atupwa jela miaka 4

Thu, 22 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Mahakama nchini Uhispania imempata mwanasoka wa zamani wa Barcelona na Brazil Dani Alves na hatia ya kumbaka mwanamke katika klabu ya usiku ya Barcelona.

Amehukumiwa kifungo cha miaka minne na nusu jela.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40, ambaye ni mmoja wa wanasoka waliovuma sana katika historia, alikana kumnyanyasa mwanamke huyo mapema saa 31 Disemba 2022.

Wakili wake aliomba kuachiliwa kwake na Alves anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Pamoja na kumhukumu Alves kifungo cha miaka minne na nusu, mahakama iliamuru amlipe fidia muathirika kiasi cha €150,000 (£128,500) na kusema anapaswa kukabiliwa na muda wa majaribio ya miaka mitano baadaye ili kuangaliwa miendendo na tabia yake.

Waendesha mashtaka walisema Alves na rafiki yake waliwanunulia shampeni wasichana watatu kabla ya kumvuta mmoja wao hadi kwenye eneo la VIP la klabu hiyo ya usiku katika choo ambacho hakulifahamu.

Waliteta kuwa ni wakati huu ambapo aligeuka kuwa mkali, na kumlazimisha mwanamke huyo kufanya ngono licha kuwasihi wamuache aondoke mara kwa mara.

Alves alikuwa amesisitiza kuwa angeweza kuondoka "kama angetaka". Lakini mahakama iligundua kuwa hakukubali.

Katika taarifa, mahakama ilisema kulikuwa na ushahidi zaidi ya ushuhuda wa mwuathiriwa ambao ulithibitisha kuwa alibakwa.

Ilisema Alves "alimshika mlalamishi ghafla" na kumtupa chini. Kisha akambaka huku akimzuia kusonga kwani "mlalamishi alisema hapana na alitaka kuondoka", iliongeza.

Mwanamke huyo alisema ubakaji huo ulimsababishia "uchungu na woga", na mmoja wa marafiki zake ambaye alikuwa naye usiku huo alielezea jinsi msichana huyo wa miaka 23 alivyoliwa kwa uchungu "bila kujizuia" baada ya kutoka bafuni.

Upande wa mashtaka ulikuwa umeomba kifungo cha miaka tisa jela. Nchini Uhispania, madai ya ubakaji yanachunguzwa chini ya shtaka la jumla la unyanyasaji wa kijinsia, na kuhukumiwa kunaweza kusababisha kifungo cha miaka minne hadi 15 jela.

Sheria ilibadilishwa hivi majuzi ili kusisitiza umuhimu wa ridhaa chini ya kanuni inayoitwa "Ndiyo tu ndio Ndiyo".

Alves aliichezea Barcelona zaidi ya mara 400, akishinda mataji sita ya ligi na Ligi ya Mabingwa mara tatu kwa misimu miwili akiwa na klabu hiyo. Pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Brazil cha Kombe la Dunia la 2022.

Chanzo: Bbc