Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dalali afunguka kilichompeleka Simba

Dalali Pic Data Dalali afunguka kilichompeleka Simba

Tue, 22 Dec 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Mwanahiba RichardMore by this Author MWENYEKITI wa zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali amefunguka juu ya uamuzi wake wa kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Swedy Mkwabi.

Mkwabi alijiuzulu nafasi hiyo Septemba mwaka jana ambapo ilikaimiwa na Mwina Kaduguda aliyepitishwa na mkutano mkuu uliofanyika Desemba mwaka jana.

Mkwabi aling’atuka madarakani akiwa ameitumikia Simba kwa mwaka mmoja pekee kwani alichaguliwa Novemba, 2018 na kwa mujibu wa Katiba ya Simba viongozi wa kuchaguliwa na wanachama hukaa miaka minne madarakani.

Akizungumza na Mwanaspoti, Dalali alisema kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kufuatwa na wanachama ambao walitumia muda mwingi kumbembeleza ili achukuwe fomu hiyo aliyoichukuwa juzi Jumamosi.

Alisema mbali na kuombwa na wanachama wa Simba, lakini ni haki ya kila mwanachama kugombea nafasi yoyote kwenye uchaguzi ili mradi awe na sifa zilizoorodheshwa ambapo yeye sifa hizo anazo.

“Ni haki ya mtu yeyote kuchukua fomu ya kugombea nafasi ndani ya Simba ili mradi tu ana vigezo na hakiuki Katiba, nimechukuwa fomu kwa kufuata kanuni za uchaguzi hivyo sipo nje ya kanuni hizo.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz