Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari alikiona kifo cha Dwamena

Raphael Dwamena Daktari alikiona kifo cha Dwamena

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daktari Antonio Asso aliyekuwa akimpa matibabu ya moyo nyota wa Ghana, Raphael Dwamena ambaye alifariki Jumamosi iliyopita baada ya kudondoka uwanjani huko Albania wakati mchezo baina ya timu yake ya Egnatia dhidi ya Partizan, amefichua kuwa mchezaji huyo aliamua kutoendelea kutumia kifaa cha kuamsha mapigo ya moyo wake ambacho kilikuwa kinamsaidia tatizo lake la moyo kusimama mara kwa mara.

Dwamena alifia njiani Novemba 11 wakati akiwapelekwa hospitalini baada ya tukio lake la kuanguka lililosababishwa na mapigo yake ya moyo kusimama na Daktari Aso amesema kuwa suala la kifo kwa mchezaji huyo lilikuwa jirani baada ya kuamua atolewe kifaa cha kuamsha mapigo ya moyo na kuendelea kucheza mpira licha ya kukatazwa.

"Dwamena amefariki kwa matokeo ya kuheshimu uamuzi wake binafsi. Lakini kama asingeagiza kifaa cha kuamsha mapigo ya moyo kiondolewe, Raphael angekuwa bado anaishi. Kuanzia wakati huo kuendelea, nilikuwa na uhakika kwamba siku moja, janga lililotokea Jumamosi kwenye uwanja wa soka Albania lingetokea.

"Tuliweza kumshawishi umuhimu wa kupandikiza kifaa cha kuamsha mapigo ya moyo ili angalau kumhakikishia maisha yake. Muda huohuo tulimshauri aache kucheza soka. Mwaka 2022, Dwamena aliomba kiamsha mapigo ya moyo kiondolewe," alisema Asso.

Kifo cha Dwamena kimesababisha kusimama kwa Ligi Kuu ya Albania na shughuli nyingine za kimichezo nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live