Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari afichua ishu ya beki Kagera kuzimia uwanjani

Daktari Kagera Afafanua Daktari afichua ishu ya beki Kagera kuzimia uwanjani

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Daktari wa Kagera Sugar, Abel Shindika amesema kitendo cha beki wa timu hiyo, Datius Peter kuzimia ni jambo la kawaida kwa mchezaji yeyote kutokana na utumiaji wa nguvu pindi anapotimiza majukumu uwanjani.

Beki huyo wa kulia alizimia ghafla uwanjani baada ya kugongana na mshambuliaji wa Mbeya City, Sixtus Sabilo dakika ya 38 wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Aprili 23 kwenye Uwanja wa Kaitaba na wenyeji kushinda bao 1-0.

Akizungumza na Mwanaspoti, Shindika alisema nyota huyo alipata mshtuko baada ya kugongwa sehemu ya goti lake kwa nyuma hivyo kumsababishia kupoteza fahamu ila baada ya kufanyiwa vipimo amegundulika hana tatizo lolote.

"Tulimpima pale pale uwanjani lakini baada ya hapo tukampeleka hospitali ya karibu kwa ajili ya matibabu zaidi na tukagundua alipata mshtuko mdogo tu ambao hauna madhara yoyote hivyo anaendelea vizuri kwa sasa," alisema.

Kwa upande wa Datius alisema lilikuwa jambo la kushtua katika maisha yake kwa sababu hali kama hiyo hajawahi kukutana nayo tangu ameanza mpira, hivyo anashukuru kwa sapoti kubwa ambayo wachezaji wenzake waliionyesha.

"Nakumbuka nilizinduka hospitalini na baada tu ya hapo kitu cha kwanza niliuliza vipi matokeo, nikaambiwa tumeshinda basi kuanzia pale nikazidi kupata nguvu mwilini na nashukuru hadi sasa naendelea vizuri," alisema.

Chanzo: Mwanaspoti