Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari Yanga afunguka hali ya Pacome

Pacome Skudu Yanga Daktari Yanga afunguka hali ya Pacome

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga, Pacome Zouzoua, baada ya kupata maumivu katika mchezo wa jana dhidi ya Singida Fountain Gate, kwa sasa yuko sawa.

Pacome alipata maumivu ya goti baada ya kugongana na mchezaji wa Singida katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC ambao Yanga waliibuka na ushindi wa magoli 2-0.

Daktari wa Yanga, Moses Etutu, amesema: “Pacome aligongana na mchezaji wa Singida na kupata maumivu ya goti, lakini baada ya kupata dawa za kutuliza maumivu amekuwa sawa.”

Pacome katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, hakumaliza dakika tisini, alitoka kipindi cha pili na kuingia Skudu Makudubela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live