Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari Yanga aeleza hali ya Aucho

Khalid Auchoooooooo Daktari Yanga aeleza hali ya Aucho

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daktari wa Yanga Moses Etutu amesema kiungo Khalid Aucho anaendelea vyema na anaweza kutumika katika mchezo unaofuata ligi kuu ya NBC dhidi ya Namungo Fc utakaopigwa Ijumaa, Machi 8 uwanja wa Majaliwa, Ruangwa.

Aucho alipata majeraha ya goti katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly. Mchezo uliopigwa Misri Yanga ikikubali kipigo cha bao 1-0.

Aucho hakuweza kumaliza dakika 90 za mchezo huo nafasi yake ikichukuliwa na Salum Abubakar 'Sure Boy'.

Etutu alisema majeraha hayo hayakuwa makubwa walichofanya katika mchezo huo ni kumpumzisha ili asipate madhara zaidi.

"Ni kweli Aucho alipata majeraha ya goti katika mchezo dhidi ya Al Ahly. Hayakuwa majeraha makubwa, tulimtoa kwa tahadhari ya kumlinda asidhurike zaidi. Yuko sawa na mwalimu anaweza kumtumia katika mchezo unaofuata," alisema Etutu.

Aucho amekuwa nguzo muhimu katika eneo la kiungo la Yanga msimu huu Ni mmoja wa wachezaji ambaye pale anapokosekana pengo lake huonekana dhahiri

Chanzo: www.tanzaniaweb.live