Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari Yanga: Wachezaji wote wako fiti, kazi kwa Gamondi

Yao Tizii Kouassi Attohoula Yao

Sat, 1 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daktari wa Young Africans, Moses Etutu, amebainisha kwamba, wachezaji wote wameanza mazoezi baada ya kikosi kufika Zanzibar na wapo vizuri kiafya.

Etutu amebainisha kwamba, licha ya kwamba wengine kwa siku za karibuni walikuwa na changamoto kidogo za kuumwa, lakini wamepata nafuu na kuungana na wenzao mazoezini.

Hayo yanajiri wakati kikosi hicho kikiwa visiwani Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Kombe la CRDB Bank dhidi ya Azam utakaochezwa Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa New Amaan Complex.

“Kwa ujumla wachezaji wapo ‘motivated’ sana, hali zao kiafya wote ni wazima, tumekuwa na wachezaji wawili mpaka wanne ambao walikuwa na shida kidogo kama kuumwa malaria na homa akiwemo Jonas Mkude lakini wameanza mazoezi vizuri, kwa hiyo tunategemea kila mtu katika timu yupo sawa na hali zao kiafya ni nzima kabisa.

“Hali ya hewa hapa ni upepo na kibaridi kidogo kulinganisha na Dar es Salaam, lakini sidhani kama hii hali ya hewa itabadilisha mabadiliko ya kimwili kwa wachezaji, pengine inaweza kutusaidia kwa sababu hali ya hewa ipo chini nyuzi joto ya Dar es Salaam.

“Hivyo basi inaweza kusaidia kupunguza uchovu na kuwafanya wachezaji wasichoke mapema, kwa hiyo ni hali ya hewa nzuri na haina madhara kwa wachezaji.

“Tunamshukuru Mungu ligi imemalizika na tumekuwa mabingwa, mechi zilikuwa zimekaribiana kwa takribani siku tatu na wachezaji wengine wamecheza mechi karibia zote.

“Kiuhalisia uchovu kwa wachezaji unakuwa mkubwa lakini tunajitahidi kukabiliana nao kwa kufanya revovery kusaidia wachezaji misuli na nyama zao kurudi kawaida na kufanya vizuri. Tunajitahidi kila liwezekanalo kusaidia na tuna vipindi tofauti vya kusaidia hali hiyo ndiyo maana tumeanza na mazoezi rahisi kuwafanya wachezaji kuwa tayari kupokea mazoezi yanayokuja,” alisema Etutu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live