Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari Yanga: Pacome yuko fiti, kazi kwa Gamondi tu!

Pacome Nzengeli Nkane.jpeg Daktari Yanga: Pacome yuko fiti, kazi kwa Gamondi tu!

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zikibaki siku mbili kabla ya kucheza na Simba SC, Mashabiki wa Young Africans wamepata habari njema kufuatia kiungo wao, Pacome Zouzoua kuanza mazoezi na wachezaji wenzake baada ya kuwa nje kwa mwezi mmoja akiuguza jeraha la nyama za paja.

Pacome anayecheza nafasi ya Kiungo Mshambuliaji, alipata jeraha hilo Machi 17 mwaka huu, wakati Young Africans ilipokubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Azam FC, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Kufuatia jeraha hilo, Pacome alikosa michezo mbalimbali ya Ligi Kuu Bara, Kombe la FA na mechi mbili za Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Akizungumza Dar es salaam, Daktari wa Young Africans anga, Moses Etutu, amesema nyota huyo raia wa lvory Coast, anaendelea vizuri na ameanza mazoezi na wenzake. "Pacome tayari ameanza mazoezi na wenzake, kuhusu kumtumia katika mchezo ujao hiyo ni kazi ya benchi la ufundi," amesema.

Keshokutwa Jumamosi (Aprili 20), Young Africans itaikaribisha Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa saa 11:00 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live