Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dakika hizi Simba hakuachi

97018 Simba+pic Dakika hizi Simba hakuachi

Wed, 26 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Simba leo inacheza na Stand United, rekodi nzuri ya kufunga mabao kipindi cha pili inaibeba timu hiyo.

Timu hizo zitacheza mchezo wa Kombe la FA kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Moto wa Simba unanogeshwa na safu ya ushambuliaji ambayo imekuwa mwiba kwa mabeki wa timu pinzani tangu ligi hiyo ilipoanza Agosti 26, mwaka jana.

Ubora wa safu hiyo unaiweka Simba katika mazingira mazuri ya kupata ushindi kulinganisha na Stand inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Kiwango bora cha Simba katika Ligi Kuu kimeipa nafasi ya kuwa kileleni kwa muda mrefu ambapo inaongoza kwa pointi 62.

Katika mechi 10 za mwisho ilizocheza katika Ligi Kuu, imeshinda michezo tisa na ushindi wao ukipatikana kipindi cha pili.

Pia Soma

Advertisement
Katika mechi tisa za ushindi, Simba imeshinda mabao 3-1 dhidi ya Biashara Mara United, imeifunga bao 1-0 Kagera Sugar na matokeo kama hayo dhidi ya Lipuli.

Pia imeichapa mabao 3-0 Mtibwa Sugar, iliinyuka 2-0 Coastal Union, iliifunga 3-2 Namungo, ilitoa kipigo 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania na ilipata matokeo kama hayo mbele ya Mbao kabla ya kuifunga Alliance 4-1.

Rekodi inaonyesha katika mechi hizo Simba imeshinda mara 21 na mabao 13 imefunga kipindi cha pili dakika ya 47, 58, 63, 72, 89, 78, 90, 57, 47, 58, 61, 68, 88 na manane kipindi cha kwanza dakika ya 35,23, 45,7,39, 22, 45 na 42.

Katika mabao hayo Kagere, Bocco na Dilunga kila mmoja amefunga manne wakati, Jonas Mkude, Gerson Fraga, Francis Kahata, Clatous Chama, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Luis Miquissone (mawili).

Simba imefungwa mabao saba, manne kipindi cha kwanza dakika ya 22, 24, 28 na 36 na matatu kipindi cha pili dakika ya 53,72 na 71.

Kocha wa Simba Sven Vanderbroek alisema amekuwa akiandaa timu kupata matokeo kulingana na aina ya mchezo husika.

Alisema amekuwa na utaratibu wa kuwaandaa wachezaji wake akiamini watafanya vyema bila kuangalia rekodi ya matokeo ya nyuma. “Sipendi kufikiria matokeo ya nyuma tunakwenda uwanjani kuikabili timu pinzani tukiwa na malengo ya kushinda,” alisema Sven.

Wakati Sven akitoa kauli hiyo, mchambuzi Ally Mayay alisema Simba inabebwa na mambo matatu ya uimara wa kikosi, kiwango bora na saikolojia ya wachezaji.

“Ni timu chache zenye uwezo kama huo nchini, hata nje mfano Manchester enzi ya Ferguson aliwajenga kisaikolojia wachezaji wake na ikawa hivyo kwamba kipindi cha kwanza wanacheza hata wasipopata bao, lakini kipindi cha pili lazima wafunge,” alisema Mayay.

Naye kocha wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni alidokeza timu ikiwa na nusu ya wachezaji wenye uwezo wa kupambana kwa kiwango kilekile kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho ina uwezo wa kufunga mabao wakati wowote katika mchezo.

Nguli huyo alisema wachezaji wamejengwa kisaikolojia kufunga mabao kipindi cha pili na wamekuwa wakifanya hivyo katika idadi kubwa ya mechi.

Chanzo: mwananchi.co.tz