Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dakika 90 za mahesabu makali kwa Stars

STARSSS 0 Taifa Stars

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

Taifa Stars inatarajia kushuka dimbani saa 10:00 jioni ya leo Novemba 11, 2021 kwenye dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam kukipiga na DR Congo kwenye mchezo wa mzunguko watano wa kundi J kuwania kufuzu michuano ya kombe la Dunia linalotaraji kuchezwa nchini Qatar 2022.

Kuelekea kwenye mchezo huo, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesema licha ya wapinzani wake  timu ya taifa ya DR Congo kupanga kuharibu mipango ya Stars, lakini Mkali huyo wa mbinu amesema anaamini wachezaji wake watawexa kukamilisha mipango na kupata matokeo mazuri.

Kim amesema, “Tunawaheshimu DR Congo ni timu nzuri, najua wamekuja kwa ajili ya kuharibu mipango yetu, lakini naamini wachezaji watacheza kukamilisha mipango yetu”.

“Tunafurahia leo tutakuwa mbele ya mashabiki wetu ambao wamekuwa nasi kuanjzia mwanzo hadi sasa katika mchezo huu, tutaingia kivingine tofauti na ule wa awali”. Alimalizia hivyo Kim Poulsen.

Kwa upande wa mwakilishi wa wachezaji, Mshambuliaji, John Rafael Bocco amesema, “Tunaingia katika mchezo huu tukiwaheshimu DR Congo, ni timu kubwa lakini tunawaomba mashabiki wetu watuombee, tunaamini tunaenda kupata matokeo”. 

Nao wapinzani wa mchezo huo, DR Congo kupitia kocha wake Hector Cuper wamejigamba kuondoka na ushindi licha ya kuwa ugenini. 

“Tuna wachezaji wengi wanaocheza nchi mbalimbali ikiwamo England, lakini hapa tunaangalia ubora wa timu nzima si mchezaji mmoja, naamini tutapata matokeo”. Kuper ambaye ni miongoni mwa makocha wazoefu na soka la Afrika amechukua mikoba ya Florent Ibenge lengo likiwa ni kufuzu michuano hiyo mikubwa Duniani.

Nae nahodhana mshambuliaji mkongwe wa DR Congo, Diumerci Mbokani ambaye aliwahi kukipigia Norwich ya England kwenye EPL, amesema ushindi ndiyo namna pekee ya kuwasaidia kusonga mbele.

“Katika nafasi tuliyopo, tunatakiwa kushinda kujiweka katika mazingira mazuri ya mchezo wa mwisho dhidi ya Benin”.

Taifa Stars ni kinara wa kundi J akiwa na alama 7 sawa na Benin, DR Congo watatu wakiwa na alama 5 wakati Madagascar anashika mkia akiwa na alama 3. Stars ikipata ushindi itafikisha alama 10 na kuwaondoa DR Congo na Madagscar kwenye uwezekano wa kufuzu tena kwani hataweza kufikia alama 10.

Chanzo: eatv.tv