Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dakika 90 za jasho na damu kwa Taifa Stars

TAIFA STAAAARZ Wachezaji wa Stars wakifanya mazoezi

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Timu ya Taifa kitajitupa Dimbani katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam Septemba 7, kutupa karata yake ya pili ya kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia Qatar 2022.

Tanzania ipo Kundi J sambamba na Benin, DR Congo na Madagascar, tayari Benin na Congo wameshashuka dimbani mara mbili huku Tanzania na Madagascar wakishuka dimbani kukamilisha idadi ya michezo miwili jioni ya leo.

kundi hilo linaongozwa na Benin mwenye alama nne (4) baada ya kushinda mchezo mmoja akimfunga Madagascar na kutoa sare na DR Congo, wakati Tanzania ilitoa sare na DR congo ugenini September 2 na leo ina kibarua kizito mbele ya Madagascar ambao kwa viwango vya ubora duniani wako nafasi ya 94 huku Tanzania ikishika nafasi ya 135.

Akizungumza wakati wa kuelekea mchezo huo , Kocha mkuu wa Stars amesema "Madagascar ni wazuri , na inatupasa tuwaheshimu wapinzani kwa kuwa wana watu wenye uzoefu ndani ya kikosi chao na walicheza robo fainali ya michuano ya AFCON".

Katika hatua hii ya makundi, mshindi wa kila kundi ndie atakaekwenda hatua inayofuata ambapo zitapatikana timu kumi na zitacheza ili kupata wawzakilishi watano ambao ndio watakaoliwakilisha bara la Afrika.

Ikumbukwe mchezo huo wa Stars pia utachezwa bila ya kuruhusu mashabiki kutokana na miongozo iliyotolewa na FIFA katika kupambana na Janga la Corona

Chanzo: www.tanzaniaweb.live