anga jana imerejea katika Ligi Kuu Bara kwa mdudu wa sare baada ya kulazimishwa suluhu na Kagera Sugar mjini Bukoba, huku nyota mpya wa timu hiyo, Joseph Guede akitumia dakika 33 uwanjani kwenye Uwanja wa Kaitaba wakati watetezi hao wakirejea kileleni mwa msimamo.
Mechi hiyo ya kwanza ya kiporo kwa Yanga, ni ya kwanza kutoka sare dhidi ya Kagera tangu ilipopoteza mara ya mwisho kwenye uwanja huo wa Kaitaba, Novemba Mosi, 2014 ilipolala 1-0, kwani wababe hao wa soka nchini walikuwa wakijipigia tu Kagera.
Sare hiyo ya jana pia ilikuwa ni kama neema kwa timu hiyo na kwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo, Fred Felix ‘Minziro’ aliyepewa shavu hivi karibuni.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha pointi 31 na kulingana na Azam inayoongoza msimamo kwa muda mrefu kabla ligi haijasimama Desemba 23 mwaka jana kupisha fainali za Afcon 2023 na michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024.
Kwa sasa Azam imebaki kileleni kutokana na kufunga mabao 35 na kufungwa 10, huku Yanga ikifunga 31 na kuruhusu sita tu nyavuni, japo Yanga ina mchezo mmoja mkononi kwani imecheza mechi 12 wakati Azam ina 13 na kwa upande wa Kagera sarev hiyo imeitoa nafsi ya 14 ya msimamo hadi ya 13 ikifikisha pointi 14 kutokana na mechi 14, ikiishusha Ihefu yenye pointi 13.
45 ZA KWANZA NGUMU
Timu zote zilimaliza kipindi cha kwanza bila kufungana, lakini zikishambuliana kwa zamu muda wote wa dakika 45 ambapo ubunifu wa eneo la mwisho la umaliziaji ulionekana kuzikwamisha, huku Yanga ikionekana kutawala zaidi mchezo.
BAO LA CHIRWA
Ukitazama marudio ya video yanakupa msaada mkubwa kwamba bao la mshambuliaji Obrey Chirwa kwa kichwa akimalizia krosi ya Ally Ramadhan lilikuwa bao halali, licha ya mwamuzi Ally Simba kudai mfungaji aliotea kabla ya kuuweka mpira wavuni.
Makosa ya mabeki wa Yanga kumsahau Chirwa ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo iliwanufaisha Kagera ingawa bao hilo likakataliwa.
Katika mchezo huo wa jana Yanga iliwaanzisha mabeki Gift Fred na Dickson Job aliyekuwa na timu ya taifa, Taifa Stars katika fainali za Afcon 2023, japo hakutumika hata kwa dakika moja katika fainali hizo za Ivory Coast.
BASI LA KAGERA
Karibu mchezo mzima Kagera Sugar walikuwa wanacheza nyuma ya mpira wakiwa na mashambulizi machache wakiwaacha Yanga kutawala mchezo huku wageni wakishindwa kuufungua ukuta wa wenyeji wao.
Yanga ilikosa ubunifu wa kuwapangua Kagera ambao walicheza kwa nidhamu kubwa wakifunga njia za kukamilisha mashambulizi ya wageni wao na kuufanya mchezo huo kuonekana kirahisi kwamba mabao yangekuwa machache.
DAKIKA 33 ZA GUEDE
Kipindi cha pili dakika ya 57 Yanga ilifanya mabadiliko mawili ikiwaingiza washambuliaji Kennedy Musonda na nyoya mpya, Joseph Guede wakichukua nafasi za Clement Mzinze na Farid Mussa.
Guede ambaye ni raia wa Ivory Coast, huo ulikuwa mchezo wa kwanza tangu asajiliwe katika dirisha dogo na jamaa huyo akifanikiwa kugusa mpira mara tano ndani ya dakika hizo mbali na zile za nyongeza kwenye mchezo huo.
Mshambuliaji huyo alipiga vichwa viwili akitumia krosi mbili, huku kichwa kimoja pekee ndio kilichokaribia kusababisha hatari lango la Kagera Sugar lililokuwa likilindwa na Ramadhan Chalamanda.
Mchezaji huyo aligusa tena mpira mara tatu nje ya eneo la hatari, lakini alijikuta yuko chini ya ulinzi mkali chini ya mabeki wawili wa kati ya