Sasa ni vita ya nafasi ya tano, baina ya Geita Gold na Namungo ambazo zimepishana pointi moja, zimecheza mechi sawa (27), jambo linalowafanya wachezaji wa timu hizo kuziona dakika 270 zilizosalia kumaliza msimu ziwe za jasho.
Geita ambao wapo nafasi ya tano wana pointi 37 huku Namungo wakiwa nafasi ya sita na pointi 36.
Baada ya Namungo FC kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba, wachezaji wa timu hiyo wanazipigia nafasi mechi tatu zilizosalia kuhakikisha zinawaweka nafasi ya tano.
Msimu uliopita Geita ilimaliza nafasi ya nne, huku Namungo ikimaliza nafasi ya tano, kitu kinachowafanya waingie kwenye bato ya ushindani kwa msimu huu tena.
Kiungo mshambuliaji wa Namungo, Jacob Masawe alisema mechi zilizosalia wanazichukulia kama fainali, kuhakikisha wanashinda zote waweze kumaliza ligi nafasi ya tano.
"Bado ligi ni ngumu kwetu, tunaihitaji nafasi ya tano ambayo inapigiwa mahesabu na Namungo, kila mmoja anapambania timu yake kwa nafasi yake.
Mchezaji mwingine aliyeunga mkono hoja hiyo ni Pius Buswita aliyesema "Kuna nafasi bado zina vita kubwa ingawa tayari zimejigawa, mfano ubingwa Yanga na Simba, nafasi ya tatu kuna Azam na SBS, tupo sisi tunaogombea nafasi ya tano, ndio maana nasema bado ligi ni ngumu kwetu,"alisema.
Kwa upande wa straika wa Geita, Elias Maguri alisema kumaliza nafasi za juu kuna heshima yake kwa wachezaji :"Japokuwa kuanzia nafasi ya nne hadi ubingwa zipo timu zilizofanikiwa kukaa kuwania eneo hilo, sisi wenyewe lazima tuipambanie hiyo ya tano."
Kocha wa Geita, , Fredy Felix 'Minziro' alisema ni suala la muda Namungo kumaliza chini yao anataka aendeleze ubabe wa msimu uliopita" Wachezaji wangu wanalijua hilo, hapa ni mapambano hadi kipyenga cha mwisho cha kumaliza msimu."