Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dakika 270 za heshima Yanga

Yanga Y00 Wachezaji wa Kikosi cha Yanga

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Yanga sasa inarudi kuendeleza rekodi yake kwenye Ligi Kuu Bara ikiwa imeshinda mechi 11 mfululizo na sasa inasaka dakika 270 ili kutetea taji lake.

Yanga inaongoza ligi kwa pointi 65 baada ya kucheza mechi 24, ikishinda 21, sare mbili na kufungwa mchezo mmoja na imebakiza michezo sita ya kutetea taji lake na kati ya hiyo ni mitatu tu itakayoamua ubingwa.

Mabingwa hao watetezi ukiachana na mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Geita Gold Aprili 7, kwenye mechi za ligi ina kibarua dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Kagera Sugar itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza kwa kipigo cha bao 1-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Baada ya dakika 90 za mchezo dhidi ya Kagera Sugar Aprili 16, Yanga itakuwa ugenini dhidi ya mtani wake, Simba ambaye yupo nafasi ya pili na mchezo huo ndio utaamua ubingwa wa Yanga kupatikana mapema au la.

Mechi dhidi ya Singida Big Stars Aprili 25, Yanga itakuwa ugenini na itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 4-1, mchezo utakaokuwa muhimu kwa pande zote mbili mmoja akihitaji kutwaa ubingwa na mwingine kuwinda nafasi ya tatu ili kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa.

WASIKIE MAKOCHA

Kocha Mecky Maxime alisema wanatarajia mchezo mgumu na wa ushindani kutokana na kukutana na timu ambayo damu yao inachemka baada ya kucheza mechi tofauti na wao wamefanya mazoezi zaidi bila ya kucheza.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu tumejiandaa kupata pointi tatu kwenye mchezo huo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri, hatujapata muda wa kucheza naamini wachezaji wangu wapo fiti watakuwa bora zaidi ndani ya dakika zote 90.

Kocha wa Singida Big Stars, Hans Pluijm alisema: “Utakuwa mchezo bora na wa ushindani kwa pande zote mbili natambua ubora wa Yanga na nimeandaa mbinu ambazo zitatupa nafasi ya kupata pointi tatu muhimu ambazo zitatufanya tuweze kuwa na uhakika wa nafasi ya tatu na umuhimu wa mechi zilizobaki si kwa Yanga tu ni mechi zote zilizo mbele yetu,” alisema Pluijm.

Juma Mgunda wa Simba alisema : “Kuna mechi mbili ngumu mbele yetu dhidi ya timu iliyo bora kuzungumzia mechi ya Yanga ni kumdharau mpinzani wetu ambaye tutakutana naye na mechi zake pia ni muhimu muda ukifika tutazungumza mchezo huo.”

Chanzo: Mwanaspoti