Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dakika 270 ngumu za Biashara united

Biashara Araaaa Kikosi cha Biashara United

Thu, 7 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kocha Mkuu wa Biashara, Patrick Odhiambo umezungumzia ugumu wa dakika 270 zilizo mbele yake na kuweka wazi wana kazi ya kufanya kuhakikisha wanafanya vizuri.

Biashara ina michezo mitatu, miwili Kombe la Shirikisho Afrika na mmoja ligi Kuu inayohitaji matokeo mazuri ili kuendelea kufanya vizuri kwenye mashindano yote.

“Nina mechi tatu ngumu hivi karibuni, naanza na Shirikisho. Tutakuwa wenyeji wa Ahli Tripol ya Libya tarehe 15 hadi 17 ndio tarehe zilizopangwa sijui hata tutacheze lini, baada ya hapo Oktoba 19 tutakuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons ugenini na 22 ni tarehe ya kurudiana na Ahli kuanzia Oktoba 22,” alisema Odhiambo na kuongeza anawaamini vijana wake watapata matokeo baada ya kushindwa kufanya vizuri michezo miwili ya kwanza ya Ligi.

Nahodha wa timu hiyo, Abdulmajid Mangaro amesema “Tukifanya vibaya kimataifa tunaondolewa hivyo kwa kuwa tunaanzia nyumbani tunatakiwa kupata matokeo mazuri kwa kufunga mabao mengi ili kupunguza ugumu ugenini.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz