Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dakika 180 zinamsubiri Okrah

Gamondi X Okrah Kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Augustine Okrah

Wed, 3 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Miguel Gamondi, amefichua kuwa winga mpya wa timu hiyo, Augustine Okraha ataonekana uwanjani katika mechi mbili zijazo za Kombe la Mapinduzi ambazo ni sawa na dakika 180.

Okrah amejiunga na Young Africans kwenye usajili wa Dirisha Dogo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Bechem United ya Ghana, alitambulishwa juzi Jumapili (Desemba 31) kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, wakati Young Africans ikicheza mechi ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Jamhuri.

Winga huyo ambaye aliwahi kuitumikia Simba SC msimu uliopita, alifanya vizuri aliporejea Ghana kuichezea Bechem United ambapo katika mechi 15 za Ligi Kuu msimu huu, alifunga mabao 9.

Chanzo: Dar24
Related Articles: