Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dakika 180 za mateso Azam FC

Azam Mateso.png Dakika 180 za mateso Azam FC

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndani ya dakika 180, ukuta wa Azam FC umeruhusu mabao sita katika mechi za Ligi Kuu Bara.

Ilianza dhidi ya Yanga 3-2 Azam FC huku mabao yote Kwa Azam FC yalifungwa na Aziz KI.

Oktoba 28 2023 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Azam FC 1-3 Namungo FC.

Mabao ya Namungo FC yalipachikwa na Pius Buswita dakika ya 10, Hasheem Manyanya dakika ya 19 na Reliants Lusajo dakika ya 50.

Bao pekee la Azam FC lilipachikwa kimiani dakika ya 70 na Ayoub Lyanga.

Ndani ya dakika 180 kwa Azam FC ni mateso kwa mashabiki kwa kuwa hawajaambulia pointi kwenye msako wa pointi sita nyumbani na ugenini. Licha ya uwepo wa nyota wake ikiwa ni pamoja na Idd Suleiman, Prince Dube, Feisal Salum ngoma ilikuwa nzito.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live