Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dah! Rais wa PSG akomaa kufukuzia saini ya Rashford

Marcus Rashford Marcus Marcus Rashford

Mon, 18 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Miamba ya soka ya Ufaransa, Paris Saint-Germain imeweka wazi dhamira yake kuu ya kuhakikisha inanasa saini ya mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford kwa gharama yoyote ile kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya.

Rashford bado ana mkataba mrefu huko Man United na kocha Erik ten Hag alisema hakuna namna yoyote ile mchezaji huyo ataruhusiwa kuondoka, lakini PSG kupitia kwa rais wake, Nasser Al-Khalaifi inaonekana kuwa siriazi kwenye mpango wa kunasa huduma ya mchezaji huyo.

Na kinachoelezwa ni kwamba mabosi wa PSG wapo tayari kupeleka ofa ya kiuchokozi huko Man United, ambayo wanaamini itabadili msimamo wa miamba hiyo ya Old Trafford na kufikiria kufanya viashahara.

Kwa kuanzia kinachoelezwa miamba hiyo ya Parc des Princes itatanguliza ofa ya Pauni 75 milioni kuona Man United wanapokeaje.

Chanzo: Mwanaspoti