Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dada wa Ronaldo aingilia kati sakata la kaka yake Man United

Dada Wa Ronaldo .jpeg Ronaldo na Ronalda

Sun, 23 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dada wa mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo ambaye ni mwanamuziki maarufu nchini Ureno, Liliana Cátia Pereira Santos Aveiro au Ronalda amedai kuwa mambo ambayo klabu hiyo na Meneja Eric Ten Hag inamfanyia kaka yake ni sawa na kusulubiwa kwa Yesu Kristo.

Ronaldo (37) aliondolewa kwenye kikosi Mashetani Wekundu kinakachomenyana na Chelsea Jumamosi jioni baada ya kugoma kucheza na hatimaye kuondoka uwanjani kabla ya kumalizika kwa mchezo wa katikati ya wiki dhidi ya Tottenham Hotspur katikati ya wiki.

Ten Hag alijibu kwa kumuondoa Mreno huyo kwenye kikosi chake dhidi ya The Blues huku Ronaldo akilazimika kufanya mazoezi peke yake huko Carrington.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live