Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dada wa Ronaldo achukizwa kaka yake kuwekwa benchi Ureno

Ronaldo Mnb Elma.jpeg Dada wa Ronaldo achukizwa kaka yake kuwekwa benchi Ureno

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dada yake wa mchezaji maarufu duniani, Cristiano Ronaldo amejitokeza kwenye mitandao ya kijamii na kukashifu uamuzi wa kocha wa timu ya taifa ya Ureno, Fernando Santos kumweka benchi kaka yake dhidi ya Uswisi.

Elma Aveiro amemkashifu Kocha, Fernando Santos huku akidai kuwa hajajua kwanini alimweka benchi Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 licha ya Ureno kupata ushindi mnono wa goli 6-1 huku mchezaji, Goncalo Ramos akipiga 'hat-trick'

''Sawa Ronaldo hata cheza milele, bahati mbaya hafungi magoli sasa ni mzee, Ureno haimuhitaji tena Ronaldo,''- ameandika Elma Aveiro

Aveiro ameandika ''Yote aliyofanya sio ya muhimu, aliyofanya yamesahaulika. Sasa wanaomba msamaha na hawamuhitaji, nitazungumza hilo baadaye. Ni haibu sana kumdhalilisha mtu ambaye amejitolea sana.''

Mwanadada huyo aliandika ujumbe kuputia Insta story katika Instagrama yake kuonyesha kukerwa kwake kwa kitendo cha kaka yake kutoanza na kutokea benchi kwa mara ya kwanza tangu kwenye michuano ya Euro 2008.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live